Muigizaji
wa Bongo movie Irene Uwoya ameonekana kuzidi kukolea kwa penzi la mume
wake Msanii wa Bongo fleva Dogo Janja kwani jana ameonyesha tattoo ya
Jina lake aliyochora.
Siku
za hivi karibuni Uwoya na Dogo Janja wameonekana kuweka mambo yao
hadharani kidogo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kukaa kimya kwa
muda mrefu tangu ndoa yao ifungwe.
Kupitia
ukurasa wake wa Instagram Dogo Janja ameanika tattoo hiyo iliyochorwa
na Uwoya kwenye maeneno ya bega iliyoandikwa Jina halisi la Dogo Janja
ambalo ni Abdul.
Dogo
Janja amemshukuru mke wake kwa kuchora tattoo ile na kumtaka amchoree
tattoo nyingine lakini safari hii iwe kwenye maeneo nyeti kabisa.



0 comments:
Chapisha Maoni