Msanii
wa Bongo movie na mfanyabiashara Jacqueline Wolper na Sarah mzungu
ambaye ni mpenzi wa Staa wa Bongo fleva kutoka WCB Harmonize wamerudi
kwenye ya vita ya mtandaoni.
Wolper
na Sarah wamerushiana maneno Kwenye mtandao wa Instagram ambapo Sarah
amemtuhumu Wolper kwa kumtumia meseji za Siri Harmonize huku akijua wazi
kabisa ni mpenzi wake.
Kupitia
ukurasa wake wa Instagram, Sarah ameandika maneno haya kumtolea povu
Wolper na kumchana kuwa anamtongoza Harmonize na kumtumia meseji huku
anaona wazi kuwa hamjibu na amemtaka Wolper aishi maisha yake.
==>Baada ya kutolewa povu hilo, Wolper alimrudishia kombora hilo Sarah na kuandika maneno haya:
Hii
sio mara ya kwanza kwa Wolper na Sarah kugombana kisa penzi la
Harmonize, siku za nyuma Sarah ameshawahi kuanika kuwa Wolper bado
anamtaka Harmonize jambo ambalo Wolper amekuwa akikataa siku zote.
0 comments:
Chapisha Maoni