Serikali imewataka wamiliki wa shule binafsi nchini kutumia
ujuzi na uzoefu wao katika nyanja ya elimu ili kuishauri Serikali nini
cha kufanya ili kiwango cha elimu inayotolewa hapa nchini kuendelea
kukua.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi,
Profesa JOYCE NDALICHAKO amesema hayo Mjini Dodoma alipokuwa akifungua
mkutano wa Chama cha Wamiliki wa shule binafsi na kuongeza kuwa ni
jukumu la jamii nzima kuhakikisha elimu nchini inakuwa.
Nao baadhi ya wamiliki wa shule binafsi wamesema kuna mambo
mengi ambayo Serikali inaweza kujifunza kutoka katika shule hizo na
kuzifanya shule za Serikali ziwe zinafanya vizuri katika mit i hani ya
kitaifa kama zilivyo za binafsi.
Mkutano wa siku moja umeshirikisha wamiliki wa shule
binafsi kutoka nchi nzima, lengo kuu likiwa ni kuangalia mafanikio na
matatizo ambayo shule binafsi nchini zinakabiliwa nazo.


0 comments:
Chapisha Maoni