Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea kukabiliana na vitendo vya uhalifu
ili kuhakikisha kuwa wakazi wa Mkoa huu wanaendelea kuwa salama na mali
zao.
Aidha
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendelea na Misako na Doria za mara
kwa mara ili kudhibiti vitendo vya uhalifu pamoja na kuzuia matukio
mbalimbali yakiwemo ya uporaji na ukabaji.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mbeya limeendesha Misako katika maeneo mbalimbali ya
Mkoa wa Mbeya baada ya kupata taarifa za uwepo wa vitendo vya uhalifu wa
kuvunja Makanisa nyakati za usiku na kuiba mali mbalimbali zilizomo
katika Makanisa.
Misako
hii ilianza mnamo tarehe 31.03.2018 na ilifanyika katika maeneo
mbalimbali ndani ya Jiji la Mbeya na katika Wilaya ya Rungwe ilifanyika
maeneo ya Kiwira na Wilaya ya Mbarali ilifanyika katika maeneo ya
Igurusi.
Katika
Misako hiyo, watuhumiwa watatu walikamatwa kutokana na kuhusika katika
matukio ya uvunjaji na kuiba Makanisani nyakati mbalimbali. Watuhumiwa
hao ni:-
- WILLIAM SANKE [23] Mkazi wa Isanga
- ELIUDI MWANSULE [28] Mkazi wa Mwakibete Viwandani
- NOA MOLELA [26] Mkazi wa Mama John
Baada
ya kukamatwa na kuhojiwa, watuhumiwa walikiri kuhusika katika matukio
ya kuvunja na kuiba Makanisani nyakati mbalimbali na mara baada ya kuiba
mali hizo huwapelekea wauzaji ambao pia wamekamatwa.
Watuhumiwa hao ni:-
Watuhumiwa hao ni:-
- HURUMA JOHN [52] Mkazi wa Igurusi Wilaya ya Mbarali
- HALID MWANGOKA [37] Mkazi wa Igurusi Wilaya ya Mbarali
- GODFREY MWALIMBA [28] Mkazi wa Mwakibete
- GWAMAKA MWAIKAMBO [32] Mkazi wa Mwakibete
Baada
ya kuhojiwa watuhumiwa wote walikiri kupokea mali hizo kutoka kwa
mtuhumiwa WILLIAM SANKE na wenzake na baada ya kuzipokea huziuza kwa
watu mbalimbali.
Misako hii imefanikisha kupatikana kwa mali mbalimbali za wizi ambazo ni:-
- Spika kubwa 15 za aina mbalimbali
- Mixer 08
- Amplifier 01
- Viti vya Plastic 108 vya rangi mbalimbali.
Watuhumiwa wote wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya na watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
Katika hatua nyingine, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kupambana na wahalifu wanaojihusisha na dawa za kulevya.
Kutokana na taarifa za kiintelijensia mnamo tarehe 11.04.2018 majira ya saa 17:00 jioni tuliweza kubaini kuwa huko maeneo ya Mlima James, Kiwanja kilichopimwa Plot Na.2590 Kitalu X Mwakibete, Kata ya Ilemi, Tarafa ya Sisimba, jiji na Mkoa wa Mbeya kuwa kuna wakulima ambao wanalima mazao mbalimbali kwa kuchanganya na miche ya Bhangi ipatayo 83.

Miche
hiyo iling’olewa na wananchi wa eneo hilo kwa kushirikiana na viongozi
wao wa Serikali za Mitaa chini ya usimamizi mkali wa Jeshi la Polisi.
Jitihada za kumtafuta mhalifu wa tukio hili zinaendelea.
WITO:
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina Msaidizi wa Polisi MUSSA A. TAIBU
anatoa wito kwa jamii kuachana na tamaa ya mali hasa kwa kujihusisha na
vitendo vya kihalifu ili wapate mali na badala yake wafanye kazi
halali.
Aidha Kamanda TAIBU anaendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukulia dhidi ya wahalifu.
Pia Kamanda TAIBU anawasihi wananchi wa Mkoa wa Mbeya na Wilaya zake kuachana na tabia ya kilimo cha Bhangi kwani watakaokamatwa watahusika wenyewe katika kuteketeza mashamba hayo lakini pia sheria kali itachukuliwa dhidi yao.

0 comments:
Chapisha Maoni