Leo
April 18, 2018 Meneja wa Ofisi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF), Miriam Zayumba na Karani wa TFF, Flora Rauya wameunganishwa
katika kesi ya jinai inayomkabili aliyekuwa Rais wa TFF, Jamal Malinzi
na wenzanke wawili.
Mahakama
hiyo inatarajia kuanza kusikiliza kesi hiyo mfululizo kwa ushahidi wa
mashahidi wa upande wa mashtaka kuanzia May 14,17 na 21, 2018.
Washtakiwa
hao wameunganishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri mara
baada ya Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leonard Swai kuomba kufanya
mabadiliko ya hati ya mashtaka.
Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao upya 30 badala ya 28 yaliyokuwa yakiwakabili awali.
Mbali
na Rais TFF, Jamal Emil Malinzi(57) wengine ni Katibu Mkuu wa TFF,
Mwesigwa Joas Selestine(46) na Mhasibu wa TFF, Nsiande Isawayo
Mwanga(27).
Katika
mashtaka hayo, Malinzi anakabiliwa na mashtaka 28 ya kula njama,
kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa
fedha wa Dola za kimarekani 173,335 na Tsh 43,100,000.
Mwesigwa anakabiliwa na mashtaka sita ya kula njama ,kughushi, kuwasilisha nyaraka za kughushi na utakatishaji fedha.
Mshtakiwa
Nsiande anakabiliwa na mashtaka mawili ya utakatishaji fedha, huku
Zayumba akikabiliwa na mashtaka tisa ya kughushi na Frola anakabiliwa na
shtaka moja la kughushi.
Baada
ya washtakiwa kusomewa mashtaka hayo walikana na upende wa mashtaka
ukadai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na wakaomba kuwasomea maelezo
ya awali.
Katika
maelezo hayo ya awali washtakiwa walikubali maelezo yao binafsi ikiwamo
majina, nafasi zao za kazi na kuyakana maelezo mengine yote.
Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi May 14,17 na 21 ,2018 kwa ajili ya kusikilizwa.
Washtakiwa
Zayumba na Flora walifanikiwa kupata masharti ya dhamana kwa sababu
mashtaka yanayowakabili yanadhamana kwa mujibu wa sheria.
Flora
aliachiwa kwa masharti ya kuwa na wadhamini 2 ambao kila mmoja alisaini
bondi ya Sh.mil 20, huku Zayumba akishindwa kutimiza masharti ya kuwa
na wadhamini 2 ambao watasaini bondi ya Sh.milion 100 kila mmoja.
0 comments:
Chapisha Maoni