test

Jumatano, 18 Aprili 2018

Polepole Amshambulia Zitto Kabwe Kwa Madai Kuwa Anapotosha Kuhusu Ripoti ya CAG....Ataka Achukuliwe Hatua


Katibu wa Halmashauri Kuu Itikadi na Uenezi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey PolePole amefunguka na kuwavaa viongozi ambao wanazungumza juu ya ripoti ya CAG na kusema baadhi ya viongozi hao wanapotosha Umma kwa kusema mambo ya uongo.

Ameagiza hatua kali kuchukuliwa dhidi ya watu wanaopotosha umma kufuatia ripoti hiyo ya CAG.

Polepole amesema hayo leo April 18, 2018 wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema wapo viongozi wa vyama vya siasa hawazungumzi juu ya mambo mazuri yaliyofanywa na serikali kama ujenzi wa miundombinu na mambo wanayopiga hatua ila wamekuwa wakidakia mambo na kutoa taarifa za uongo.

 ”Kuna mtu mmoja anaongoza kwa upotoshaji juu ya ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG. Chama chake kina mbunge mmoja tu wa ACT Wazalendo. Sijui kasoma shule gani huyu. Kaja anasoma juu juu tu eti trilioni 1.5. Ana bahati ndugu Magufuli ni mpole ila tushawambia mwaka 2020 akatafute kazi ya kufanya. Pia arudi shule akasome kwani hakuna shilingi moja iliyopotea.

"Tunaweza tukakwambia tusaidie kuthibitisha sasa ukishindwa umesema uongo umeuhadaa Umma, umetoa takwimu za uongo ukichukuliwa hatua sio ndiyo utaanza kusema uongozi huu hatuna huruma, huruma kwa watu waovu? Waongo wanaopotosha kwa makusudi hilo halikubaliki".

Polepole katika mkutano huu ameeendelea kumtuhumu Zitto Kabwe  kushindwa kuwa na uhakiki wa maneno yake

"Kuna kipindi mtu huyu alizungumza kuhusu njaa, wewe unaijua njaa inatangazwa vipi sasa tumevumilia sana leo tumeshindwa tumeona tumsaidie kumuelewesha halafu tuseme wale ambao wana dhamana ya kuhakiki maneno tunayatoa kwa kweli wachukue hatua kwani hatupo tayari kuacha watu wachache waendelee kuudanganya umma wa watanzania hili halikubaliki" alisisitiza

Mwisho wa wiki iliyopita, Mbunge wa Kigoma Mjini kwa triketi ya ACT Wazalendo, Zitto Kabwe aliizungumzia kwa mapana zaidi taarifa ya CAG na kuonyesha mambo ambayo serikali imetuhumiwa kufanya ikiwa pamoja na upotevu wa fedha zaidi ya Trilioni 1.5 ambayo haina maelezo imetumikaje.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni