Wasanii
Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Faustina Charles ‘Nandy’ wamehojiwa
kwa saa mbili na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).
Wakizungumza
mara baada ya kumaliza mahojiano hayo yaliyofanyika leo Aprili 19,
wasanii hao wamesema wamejifunza mengi kuhusiana na masuala ya mitandao.
Diamond
amesema: “Ujana ni maji ya moto tumeelimishwa, hatutarudia tena,
nitakuwa balozi kwa vijana wenzangu kuhusu masuala ya mitandao.”
Nandy amesema: “Nisameheni kwa yaliyotokea. Hapa TCRA nimepata somo kuhusu mitandao, tukio lile halitajirudia tena.”
0 comments:
Chapisha Maoni