Makonda
ameyasema hayo leo Aprili 19, katika uzinduzi wa hospitali ya kisasa ya
mama na mtoto iliyopo Chanika iliyojengwa kwa msaada wa Shirika
Maendeleo la Kimataida la Korea (Koica).
“Eti
wanasema navunja sheria, natakiwa nifanye faragha kama unataka faragha
tunza mtoto. Mimi siogopi, nipo tayari kufungwa lakini kwa ajili wa
kutetea haki za watoto. Pengine hao wanaosema navunja sheria wana watoto
wao nje wanaogopa kujitokeza,” amesema.
Jana,
Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi akiwa bungeni
alisema kampeni hiyo inaweza kuleta hali ya sintofahamu na akabainisha
kuwa inapaswa kufanyika faragha na sio kama inavyofanyika sasa.
Awali,
Waziri wa Afya, Jinsia, Wanawake na Watoto, Ummy Mwalimu alisema
kampeni hiyo ni sahihi ila kasoro yake ni kutokuwa na faragha, lakini
akasema kwa sasa inafanyika huku picha za watoto zikifichwa.
Aliyeibua
hilo bungeni jana alikuwa ni mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga
aliyehoji uhalali wa kampeni hiyo na akahoji kama haivunji sheria na
kuwavunjia haki wanawake na watoto.
0 comments:
Chapisha Maoni