Spika
wa Bunge, Job Ndugai amesema ili mbunge aweze kutibiwa nje ya nchi kwa
gharama za Bunge anapaswa kuwa na vibali vitatu; kibali cha Bunge,
Hospitali ya Taifa Muhimbili na Rais John Magufuli.
Ametoa
kauli hiyo wakati akijibu mwongozo wa Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema),
Godbless Lema aliyehoji sababu za Bunge kushindwa kutoa gharama za
matibabu za mbunge wa chama hicho Singida Mashariki, Tundu Lissu.
"Kuna
siku nitataja orodha ya wabunge wanaotibiwa nje ya nchi. Ni lazima wawe
na vibali hivi. Rais alishasema wazi kuwa anazuia safari za nje
zisizokuwa na lazima. Lissu alipelekwa Nairobi katika matibabu kwa
utaratibu ambao haukuwa na kibali cha Bunge. Hili jambo nimeshalisema
sana sijui kwanini linajirudia, "amesema na kuongeza:
“Nashukuru Lissu anaendelea na matibabu na ninajua kuna Wajerumani wanamsaidia."
0 comments:
Chapisha Maoni