Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linawashikilia watu 27
wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema kwa tuhuma za kufanya fujo katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi ya viongozi wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ikiendelea mahakamani hapo.
Kwa
mujibu wa Kamanda Mambosasa wanaoshikiliwa ni wanaume 20 na wanawake
saba, ambao walikamatwa katika eneo la Mahakama hiyo wakifanya fujo
wakati wakisubiri uamuzi wa Mahakama hiyo juu ya hatima ya dhamana
viongozi hao saba wa Chadema.
“Watu
hao walikuwa wanafanya vurugu katika eneo la Mahakama wakati Mahakama
inaendelea, tumewashikilia na tutawafikisha mahakamani tukikamilisha
taratibu,” alisema Mambosasa.
0 comments:
Chapisha Maoni