Jeshi
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia Mbunge wa
Tarime Vijini, John Heche (Chadema), kwa tuhuma za kushindwa kuripoti
polisi kama alivyotakiwa na jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitishwa kushikiliwa kwa mbunge huyo tangu jana.
Mambosasa
amesema Heche alikamatwa kwa kosa sawa na lile lililokuwa likimkabili
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, ambaye pia alishindwa kuripoti polisi wiki
iliyopita baada ya kwenda Afrika Kusini kwa matibabu kabla ya kukamatwa
Uwanja wa Ndega wa Dar es Salaam (JNIA), usiku wa kuamkia juzi.
Aidha,
Mambosasa amesema endapo taratibu zitakamilika mbunge huyo anaweza
kufikishwa mahakamani leo, kuunganishwa katika kesi ya viongozi wengine
wa chama hicho waliopata dhamana jana.
“Ni
kama alivyoshikiliwa mwenzake Mdee naye hakuripoti, walikuja wakatakiwa
kurudi wote wao hawakurudi, hakuna kosa jipya kosa lake ni kutorudi
hadi wenzake wanapelekwa mahakamani,” amesema Mambosasa.
Machi
27 mwaka huu Heche alishindwa kuripoti polisi pamoja na viongozi
wengine saba wa chama hicho kama walivyotakiwa na jeshi hilo akidai
alikuwa na msiba.
Viongozi
hao ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa chama
hicho, Vincent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, Naibu
Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji
Peter Msigwa na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko ambao wanakabiliwa
na mashtaka manane yakiwamo kuhamasisha maandamano, uchochezi na uasi.
0 comments:
Chapisha Maoni