Kampuni
ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania Plc inapenda kuwataarifu wateja
wake na Watanzania kwa ujumla kwamba, itaendelea kutoa huduma ya ununuzi
wa umeme (LUKU) kupitia mfumo wa malipo wa serikali ujulikanao kama
Government e-Payment Gateway (GePG).
Kufuatia
mabadiliko yaliyotangazwa hivi karibuni na kampuni ya kuzalisha na
kutoa huduma ya umeme nchini (TANESCO) kuhusu kuanza kutoa huduma ya
kununua umeme kwa kupitia mfumo wa Serikali wa GePG, Vodacom Tanzania
Plc inapenda kuwatoa hofu Wateja wake kwamba wataendela kupata huduma ya
kununua umeme ya LUKU kupitia Vodacom M-Pesa kama ilivyokuwa mwanzo.
Mfumo
mpya utaiwezesha Tanesco kuunganisha mauzo moja kwa moja kutoka
makampuni mengine ya simu na mabenki kwenda GePG ikiwa ni matakwa ya
sheria kwa taasisi za Serikali.
Kutakuwa
na ongezeko la asilimia moja nukta moja ya gharama halisi (1.1%)
anayotozwa mteja ili kununua umeme pindi atumiapo huduma ya M-Pesa.
Vodacom
inawahakikishia Wateja wake kwamba itaendelea kutoa huduma ya LUKU
kupitia M-Pesa ambayo pia inapatikana katika App za Apple, na Android.
0 comments:
Chapisha Maoni