Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za
mafunzo ya muda mrefu kutoka Kamisheni ya Umoja wa Afrika
yatakayofanyika katika Chuo Kikuu cha Pan African (PAU).
Mafunzo
hayo ambayo yapo kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili na Shahada ya Uzamivu
yatatolewa katika kozi mbalimbali zikiwemo Baiolojia, Hesabu, Uhandisi,
Sayansi ya Afya, Usimamizi wa Mazingira, Sayansi ya Michezo, Mifugo,
Uongozi na Mtangamano, Lugha, Ukalimani wa Mikutano na Ufasiri, Uhandisi
wa Maji na Nishati.
Kwa
waombaji wa Shahada ya Uzamili wanatakiwa kuwa na miaka isiyozidi 30
kwa waombaji wanaume na miaka isiyozidi 35 kwa waombaji wanawake.
Aidha, kwa waombaji wa Shahada ya Uzamivu wasiwe na miaka zaidi ya 35
kwa waombaji wanaume na miaka isiyozidi 40 kwa waombaji wanawake.
Maombi ya mafunzo haya yanatakiwa kufanyika kwa njia ya mtandao (online) kupitia anuani ya barua pepe ya pau-au.net.
Mwisho
wa kutuma maombi ya fursa hizi ni tarehe 20 Aprili, 2018. Maelezo ya
ziada kuhusu mafunzo haya yanapatikana kupitia
pau.scholarships@africa-union.org au www.pau-au.net. Mratibu wa Mafunzo
haya ni Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje Na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
18Aprili, 2018
0 comments:
Chapisha Maoni