Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Susan
Kolimba amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EALA) Mhe. Martin Ngoga katika Ofisi za Wizara hiyo
mjini Dodoma.
Katika
mazungumzo yao Dkt. Kolimba amemwahidi Spika wa EALA kuwa, Wizara na
Serikali kwa ujumla itatoa ushirikiano wa hali ya juu kwa Bunge hilo
katika utekelezaji wa majukumu yake ikiwa na lengo la kuboresha
ushirikiano baina ya nchi wanachama wa EALA.
Kwa
upande wake Spika wa EALA amesema kuwa, kwa sasa wamejipanga vizuri
katika kuhakikisha wanadumisha ushirikiano na Mabunge ya Nchi wanachama
na kutoa mrejesho kwa Nchi wanachama kuhusu masuala mbalimbali ya
yanayojili katika Bunge hilo.
Spika
Ngoga yupo Mkoani Dodoma ambapo Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki
linaendelea na vikao vyake mjini humo ambavyo vimeanza April 9 na
vinatarajiwa kumalizika April 28


0 comments:
Chapisha Maoni