test

Jumamosi, 14 Aprili 2018

Mbunge wa CCM apiga magoti bungeni kumshukuru Rais Magufuli kwa kupeleka maendeleo wilayani kwake


Mbunge wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Janeth Mbene amepiga magoti bungeni na kumshukuru Rais John Magufuli kwa kupeleka maendeleo kwenye wilaya yake anayodai ilisahaulika.

Mbene amefanya kitendo hicho jana  Aprili 13, 2018
bungeni  wakati akichangia bajeti ya Ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Mara baada ya kuruhusiwa kuchangia bajeti hiyo, Mbene amesema wilaya ya Ileje ni ya miaka mingi lakini ilikuwa haina barabara ya lami lakini katika Serikali ya awamu ya tano, barabara imejengwa.

Katika kuonyesha kuwa jambo hilo limemfurahisha, mbunge huyo alipiga magoti pembeni ya kiti anachoketi bungeni akimshukuru Rais Magufuli.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni