Serikali
imesema haina mpango wa kurejesha kwa wananchi eneo la ardhi katika
Gereza la Matongo kama ilivyoombwa na Mbunge wa Bariadi Mashariki,
Andrew Chenge.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema leo Aprili 19
bungeni na kueleza kuwa gereza hilo lililopo mkoani Simiyu katika
Wilaya ya Bariadi lenye ukubwa wa eka 2,472.62 bado lina umuhimu wake
hasa katika shughuli za kilimo.
Masauni
amesema gereza hilo lilianzishwa mwaka 1975 kwa kuchukua eneo
lililokuwa la mbunge wa zamani wa Bariadi, Edward Ng'wani (marehemu)
ambaye alifidiwa eneo jingine la Serikali.
"Gereza
la Matongo lililopo mkoani Simiyu katika wilaya ya Bariadi lenye ukubwa
wa ekari 2472 lilianzishwa mwaka 1975, baada ya kuchukuliwa eneo hilo
lililokuwa eneo la Mbunge wa enzi hizo Edward Mwani ambaye alifidiwa
eneo jingine na serikali.
"Kwa
serikali ipo kwenye mpango wa kuboresha kilimo kupitia jeshi la
magereza kwa kuliwezesha kuzalisha chakula cha kutosheleza kulisha
wafungwa na mahabusu hivyo eneo la Matongo lipo kwenye orodha ya maeneo
yaliyopewa kipaumbele katika kilimo cha mahindi, alizeti, pamba, ufugaji
wa nyuki na mifugo pamoja na upandaji wa miti na uhifadhi wa
mazingira,
"Serikali
ilichukua eneo hilo ili kuwezesha magereza kuendeleza shughuli za
uelimishaji wa wafungwa kwa kutumia kilimo na ufugaji kwa sasa eneo hili
limepimwa na taratibu za kupatikana kwa hati zinaendelea hivyo serikali
haina mpango wa kurejesha eneo hilo kwa vijiji tajwa" alisisitiza
Masauni
Majibu ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni yalimuinua tena Andrew Chenge na kutaka kufahamu ni lini serikali itakuwa tayari kuanza mpango huo kwani ni miaka mingi imeshindwa kufanya hivyo.
"Mhe. Spika gereza na Matongo ni gereza ambalo ni miongoni mwa magareza yaliyoanzishwa na serikali katikati ya miaka ya 70 kwa lengo hilo hilo ambalo waziri amelisema lakini zaidi ya miaka 40 ukifika pale Matongo hakuna cha maana kinachoendelea na Mhe.

"Waziri
katika majibu yake anasema gereza hili lipo kwenye mpango wa kuboresha
kilimo sasa ni lini mpango huu mahususi kwa gereza la Matongo utaanza
kutekelezwa na serikali" alihoji Andrew Chenge
Awali, Chenge aliiomba Serikali kama itakuwa tayari kurejesha eneo la gereza hilo kwa wananchi wa vijiji vinavyolizunguka.
Naibu
Waziri Masauni amesema wananchi wa vijiji vya Mwanchumu na Salaliya kwa
asili yao si wenyeji, bali ni wahamiaji kutoka maeneo mengine.
Amesema
Serikali ilitwaa eneo hilo ili kuliwezesha Jeshi la Magereza kuendeleza
shughuli za urekebishaji tabia wafungwa na mahabusu.
0 comments:
Chapisha Maoni