Na: Lilian Lundo – MAELEZO, Dodoma.
Kamati
za maafa za Mikoa na Wilaya kufanya tathimini ya kujua miundombinu
iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea kunyesha hapa nchini ili hatua
stahiki ziweze kuchukuliwa.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa
akijibu swali la Mhe. Hussein Nassor juu ya mpango wa serikali
kurejesha miundombinu iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea nchini.
“Kipindi
hiki tumeendelea kupata mvua nyingi nchini, ambazo zimesababisha maafa,
Nawapa pole wale waliopoteza ndugu zao na kuharibiwa na miundombinu
kutokana na mvua hizo,” alisema Waziri Mkuu.
Amesema,
Serikali inaendelea kujipanga kuhakikisha miundombinu yote
iliyoharibiwa na mvua zinazoendelea inarejeshwa katika hali yake kupitia
kamati za maafa za mikoa na wilaya kwa kushirikiana na Wakala wa
Barabara Tanzania (TANROADS) pamoja na Wakala wa Barabara Mijini na
Vijijini (TARURA).
Hata
hivyo, amewataka wakulima kutumia mvua zinazoendelea kunyesha kwa
kulima mazao ya chakula na biashara kwani Serikali imejipanga vyema
kushirikiana na wakulima kutafuta masoko ya mazao hayo ndani na nje ya
nchi.
Aidha
Waziri Mkuu, ametoa wito kwa wananchi wanaoishi mabondeni kuhama kwani
mvua zinazoendelea kunyesha zinaweza kuleta madhara makubwa zaidi ikiwa
ni pamoja na kupoteza maisha.
Vile
vile Mhe. Majaliwa amesema, Serikali imetoa shilingi Bilioni 160 kwa
ajili ya kujenga na kuimarisha vituo vya afya ngazi za wilaya nchi nzima
ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Serikali kuimarisha huduma za afya hapa
nchini.
Ameendelea
kwa kusema, lengo la Serikali ni kuhakikisha vituo hivyo vya afya
vinakuwa na chumba cha maabara, chumba cha upasuaji pamoja na chumba kwa
ajili ya huduma ya mama na mtoto.
Amesema, ujenzi huo wa vituo vya afya unaenda sambamba na ujenzi wa nyumba ya mganga mkuu katika kila kituo.
Bunge
la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeweka utaratibu wa wabunge wa
bunge hilo kumuuliza maswali ya papo kwa papo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa kila siku ya Alhamisi katika
mikutano yote ya Bunge.


0 comments:
Chapisha Maoni