Serikali
ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto nchini imesema haina mpango wa kuweka vifaa vya CT SCAN
katika hospitali za ngazi ya rufaa kwenye mikoa kutokana na vifaa hivyo
kuwa na gharama kubwa pamoja na kutokuwepo kwa wataalam wa kuvitumia
Kauli
hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Dkt. Faustine Ndugulile
leo Aprili 27, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 18 mkutano wa
11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la
nyongeza la Mbunge kiza Hussein Mayeye aliyetaka kufahamu ni lini
serikali itaweza kupeleka vifaa vya CT SCAN pamoja na vile vya kupimia
saratani ya shingo ya kizazi katika hospitali ya Maweni iliyopo mkoani
Kigoma.
"Kwa
mujibu wa mpango wa serikali na aina ya huduma ambazo zinazotolewa sasa
hivi katika hospitali ngazi za rufaa za mikoa hatuna mpango wa kuweka
CT SCAN kwasababu vifaa hivyo kuwa na gharama kubwa pamoja na kuhitaji
utalaamu wa hali ya juu ambapo ngazi za rufaa za mikoa hawana", amesema
Dkt. Ndugulile.
Pamoja
na hayo, Dkt. Ndugulile ameendelea kwa kusema "sasa hivi katika
mikakati yetu mashine za CT SCAN zitapatikana kuanzia ngazi ya rufaa za
kanda lakini vipimo kwa ajili ya dalili za awali za saratani ya shingo
ya kizazi vifaa hivi vyote vinapatikana hadi katika ngazi ya vituo vya
afya na nitoe rai kwa wananchi na Wabunge kuwa huduma hizi zinatolewa
zaidi ya vituo 1,000 ndani ya nchi ya Tanzania".
Kwa
upande mwingine, Dkt. Faustine Ndugulile amesema wizara yake inaendelea
kushirikiana na mamlaka katika ngazi za mkoa na halmashauri kuhakikisha
kwamba mikakati yote waliyoiweka katika kutokomeza ugonjwa wa
kipindupindu inaendelea kufanyika kwa maana kutolewa kwa elimu pamoja na
vipimo na dawa.
0 comments:
Chapisha Maoni