Kamati
ya Rufaa ya Maadili ya TFF imetupilia mbali rufaa ya aliyekuwa makamu
wa Rais wa shirikisho hilo Ndg. Michael Wambura aliyefungiwa maisha
kutojihusisha na soka mapema mwezi Machi.
Taarifa
ya TFF leo, imeeleza kuwa baada ya kupitia hoja zake za kukata rufaa
kamati imejiridhisha na maamuzi ya awali yaliyotolewa na Kamati ya
Maadili ya kumfungia Maisha.
Machi
14 Wambura akiwa Makamu wa Rais wa TFF alifikishwa kwenye kamati hiyo
kwa masuala ya kimaadili, akikabiliwa na makosa matatu kupokea fedha za
shirikisho malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya
Shirikisho.
Machi
15 Kamati ya Maadili ya TFF ilimfungia Michael Wambura kifungo cha
kutojihusisha na mpira wa Miguu maisha kwa mujibu wa kifungu cha 73(1)
(c) cha Kanuni za Maadili ya TFF Toleo la 2013. Baada ya kupatikana na
makosa matatu.
Mara
kadhaa Wambura amekuwa akijitokeza hadharani na kuweka wazi kuwa
hakubaliani na maamuzi hayo kwani hakupewa nafasi ya kujitetea na
aliamua kukata rufaa lakini nayo imetupiliwa mbali leo.
0 comments:
Chapisha Maoni