Mbunge
wa Misungwi, Charles Kitwanga (CCM), amedai vitambulisho vya wabunge
vina kamba ambazo baadhi ya wabunge wanaweza kuzitumia kujinyonga hivyo
viondolewe.
Akiomba
mwongozo bungeni leo Ijumaa Aprili 6, Kitwanga amesema kutokana na hali
hiyo ni kwanini Bunge lisione umuhimu wa kutumia vitambulisho vya
kisasa badala ya hivyo.
“Maana
hivi vina kamba ambazo nina wasiwasi watani wangu kama Lukuvi (Waziri
wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na wahehe wanaweza kujinyonga,”
amesema Kitwanga.
Akijibu
mwongozo huo, Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge amesema ni lazima
waende na wakati kwa kutumia vitambulisho vya kisasa ambavo ni hivyo.
0 comments:
Chapisha Maoni