Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema
kuwa anajua wapo watakaotumika kuleta vikwazo kwenye hatua anazopiga za
kuiletea maendeleo nchi.
Ameyasema
hayo jana katika uzinduzi wa jengo la PSPF mkoani Dodoma, ambapo Rais
Dkt. Magufuli alisema kwamba wapo ambao hawapendi kuona Tanzania inapiga
hatua kwenye uchumi, hivyo watu watatumika na mabeberu kuleta
vipingamizi na vikwazo, lakini yeye ataendelea kuchapa kazi kwa ajili ya
watanzania masikini.
“Katika
juhudi hizi za kuleta maendeleo wapo wengine watasaliti njiani, wapo
wengine watatumika na mbinu za mabeberu, na hasa katika masuala haya ya
kujenga nchi yetu, na hasa kwa sababu nchi yetu inakwenda mbele, ni
lazima itawakwaza wengine, katika jukumu lolote la kazi hata kwenye
familia, lazima watapatikana wa kupinga pinga kidogo, lakini kikubwa ni
kunyoosha mstari kwa ajili ya kuwatumikia Watanzania masikini”, alisema
Rais Dkt. Magufuli.
Sambamba
na hilo, Rais Magufuli amemuhakikishia mtoto wa Baba wa Taifa Mwl. JK
Nyerere, Makongoro Nyerere, kuwa nchi ipo salama na imara, na anaamini
itafika ikiwa imara zaidi licha ya vikwazo vingi anavyokutana navyo.
0 comments:
Chapisha Maoni