Tanzania
na Israel zimekubaliana kwamba , mataifa hayo mawili yana mengi ya
kujifunza baina yao hususani katika eneo la utoaji wa haki na
usimamiaji wa sheria.
Hayo
yamejiri jana ( jumatatu) wakati Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk.
Adelardus Kilangi, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa
Sheria wa Israel Bi. Ayalet Shaked.
Katika
mazungumzo hayo yaliyofanyika katika Jengo la Mikutano la Kimataifa
la Mwalimu Julius Nyerere ( JNICC), viongozi hao walikubaliana kwamba
kuna haja na umuhimu wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa Tanzania na
Mwanasheria Mkuu wa Israel kukutana kwa lengo la kuainisha maeneo
ambayo Ofisi hizo mbili zinaweza kushirikiana.
“
Nadhani tuna mengi ya kujifunza kutoka kwenu na halikadhalika nanyi
kuna maeneo ambayo mnaweza kujifunza kutoka kwetu. Hivyo basi,
ninaamini kwamba pale itakapowezekana, kuna umuhimu wa mimi kukutana
na mwenzangu ili tuweze kuangalia maeneo ya kipaumbele ambayo tunaweza
kubadilishana uzoefu na kupanua wigo wa ushirikiano baina ya nchi
zetu”, akasema Dk. Kilangi.
Akayataja
maeneo ambayo anaamini Tanzania na Israel zinaweza kushirikiana ni
pamoja na namna bora ya kuimarisha mifumo ya utoaji haki na
ushauri wa kisheria wenye tija, pamoja na eneo la uwezeshwji ( capacity
building).
Mwanasheria
Mkuu , Dk. Kilangi ambaye alifuatana na Naibu Mwanasheria Mkuu wa
Serikali Bw, Edson Athnas Makallo, aliyatumia mazungumzo kati yake
na Waziri Shaked kuelezea baadhi ya majukumu yake anayoyatekeleza
kama Mshauri Mkuu wa Serikali katika masuala yote yanayohusu sheria
pamoja muundo mpya wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu ambao umehusisha
kuanzishwa kwa Wakili Mkuu wa Serikali.
Kwa
upande wake, Waziri wa Sheria wa Israel, ambaye Tanzania inakuwa
nchi yake ya kwanza kutembelea Barani Afrika, pamoja na kukubaliana na
wazo la Dk. Kilangi la kuangalia uwezekano wa Wanasheria Wakuu
kukutana katika muda utakaopangwa. Amesema kwamba, Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali ni Ofisi nyeti na yenye hadhi ya juu kabisa
katika nchi yoyote ile ikiwamo Israel.
Akaongeza
kwamba, majukumu anayoyatekeleza Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk.
Adelardus Kilangi yanashabihiana na anayotekeleza Mwanasheria Mkuu
wa Israel yakiwamo ya kuisimamia serikali katika masuala yote
yanayohusu sheria, kuiwakilisha serikali katika mahakama za juu na
mahakama za chini pamoja na kuendesha mashauri ya jinai hivyo wawili
hao wakipata fursa ya kukutana bila shaka watakuwa na mengi ya
kujadiliana na kushirikiana.
Waziri
wa Sheria wa Israel Ayalet Shaked anaongoza ujumbe wa wafanyabiashara
kutoka Israel ambao upo hapa nchini kukutana na wafanyabiashara wa
Tanzania.
0 comments:
Chapisha Maoni