test

Jumatatu, 25 Mei 2015

Sakata la Picha Za UCHI......Shilole Awaomba Radhi Wanawake Kwa Kuwadhalilisha




Baada ya wiki kadhaa kupita tangu picha zake zisambae zikimuonesha gauni likiwa limevuka nakuachia maziwa wazi, staa wa Bongo Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ameibuka na kuwaomba radhi kinamama wote. 
 
Shilole amesema kuwa anajua kwamba kitendo hicho kimewakwaza wengi na hakukusudia kufanya jambo kama lile. 
 
“Nimejifunza mengi na naendelea tena kuomba msamaha kuwa tatizo hili halitajitokeza tena ,niwaombe radhi kina mama na mashabiki wangu,” alisema.
 
Shilole alifanya tukio hilo alipokuwa jijini Antwepen, Ubelgiji kwenye shoo ambapo aliongozana na mpenzi wake,Nuh Mziwanda.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni