Rais John Magufuli leo ametoboa siri kuwa mke wake, Janeth alikuwa ni mtoto wa polisi.
Ameyasema
hayo leo Aprili 7 wakati wa uzinduzi wa nyumba 31 za polisi mjini
Arusha na kusema baba mkwe wake alikuwa sajenti wa polisi.
“Nyumba
za polisi ndizo zimenipa mke kwa hiyo nyumba za polisi ninazifahamu,
huyu mke wangu niliye naye alikuwa mtoto wa polisi, marehemu baba yake
hakuwa na cheo kikubwa alifariki akiwa sajenti,” amesema.
Ameongeza
kuwa, “Ingekuwa nazindua Moshi, angenionyesha nyumba walizokaa lakini
za Oysterbay alizoishi alishanionyesha na za Ukonga na za sehemu
nyingine. Kwa hiyo maisha ya polisi ninayafahamu.”


0 comments:
Chapisha Maoni