Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewataka
jeshi la polisi kufanya lolote lililopo ndani ya uwezo wao, ili
kuhakikisha mani ya nchi haivunjwi na kubaki na utulivu.
Kauli
hiiyo imetolewa leo jijini Arusha alipokuwa akihutubia kwenye uwanja wa
Sheikh Amri Abeid, na kusema kwamba anatambua kazi ya jeshi la polisi
ingawa kuna watu ambao wana wabeza, hivyo wasiyumbishwe na watu hao, ila
waendelee kuchapa kazi kwani yeye kama Amiri Jeshi Mkuu wao yuko pamoja
nao.
“Kuna
watanzania wanaongea maneno ya kebehi kebehi kuhusu polisi, hawajui
thamani ya polisi, ndugu zangu polisi tembeeni kifua mbele, na kwa
bahati nzuri mimi ni shemeji yenu, mkwe wenu, msiwe na wasi wasi, maneno
ya kashfa na kebehi yanayozungumzwa na wengine wala yasiwakatishe
tamaa.
"Nilipopewa
urais nikaapa kuhakikisha nchi inakuwa salama, na kuhakikisha nchi
inakuwa salama, lazima jeshi la polisi liwe salama, endeleeni kuilinda
amani ya nchi yetu, mtakayoyaamua yaamueni na mimi nitawasapoti, niliapa
kuilinda amani ya nchi hii kwa nguvu zote na nitailinda”, amesema Rais
Magufuli.
Sambamba
na hilo Rais Magufuli amesema anatambua mazingira magumu waliyonayo
askari polisi hususan wa vyeo vya chini, hivyo atahakikisha anatatua
kero zao ikiwemo kuboresha makazi yao.


0 comments:
Chapisha Maoni