Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema
serikali itawafikisha Mahakamani na kuwafutia hati ya umiliki wananchi
wote wanaomiliki ardhi ambao wamekuwa hawalipi kodi ya ardhi.
Lukuvi
ametoa kauli hiyo mara baada ya kupokea taarifa mbalimbali kutoka kwa
watendaji wake ambapo amesema serikali inapoteza mapato mengi kwa kuwa
baadhi ya wananchi kukosa uaminifu wa kulipa kodi ya ardhi kwa wakati.
Kutokana
na hali hiyo, Waziri Lukuvi amesema ameamua kutoa muda hadi Aprili 30,
2018 ili kila mtu anayemiliki ardhi awe amekwisha lipa kodi hiyo na kwa
wale ambao hawatalipa kodi kwa wakati ni wazi serikali itawafikisha
mahakamani, kuwafutia hati za viwanja hivyo na kuviuza upya kwa wamiliki
wengine ama kuuza nyumba zao.
Aidha
Mhe. Lukuvi amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuhakikisha
wanashiriki kikamilifu katika zoezi hilo ili kupunguza ukubwa wa kazi na
kukusanya fedha kwa wakati na kuongeza pato la taifa.


0 comments:
Chapisha Maoni