Rais
John Magufuli amesimulia mara ya kwanza alipopelekwa mkoani humo kusoma
kwamba hakula nyama kwa mwezi mmoja baada ya kutahadharishwa na watu
kuwa akifika asile kitoweo hicho.
Akihutubia
wakazi wa Iringa wakati wa ufunguzi wa barabara ya Iringa-Fufu jana
Aprili 29, 2018; Rais Magufuli alisema alifika Iringa kwa mara ya kwanza
mwaka 1978/79 kwa ajili ya masomo katika Sekondari ya Mkwawa.
“Niliambiwa
usile nyama, usile mshikaki Iringa na kweli sikula," alisema na kwamba,
baada ya kukaa muda alibaini wakazi wa Iringa hasa wanaume kuwa ni
wakarimu.
"Wanaume
wa Iringa ni wapole sana, unamchokoza lakini anajinyonga yeye badala ya
kukuadhibu wewe," aliongeza Rais Magufuli huku akishangiliwa na umati
wa wananchi.
Anasema watu wa Iringa ni tofauti na wenzao wa mkoani Mara ambao ukiwachokoza utakiona cha mtema kuni.
0 comments:
Chapisha Maoni