Kamanda
wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema msanii
Naseeb Abdul maarufu Diamond Platinumz jana Jumatatu Aprili 16
alishikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano kufuatia kusambaza picha
zisizo na maadili.
Mambosasa
amesema kuwa Diamond alihojiwa na kupewa dhamana jana Jumatatu huku
uchunguzi zaidi ukiwa unaendelea na utakapokamilika ataitwa tena polisi.
“Alihojiwa jana na akapewa dhamana, upelelezi unaendelea,” amesema Mambosasa.
Leo
katika kipindi cha maswali na majibu bungeni, Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amesema polisi
inamshikilia msanii huyo na Nandy ambao kwa nyakati tofauti wanadaiwa
kusambaza picha sisizo na maadili kwenye mtandao.
Wasanii hao wanadaiwa kusambaza picha hizo kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram.


0 comments:
Chapisha Maoni