Wiki
iliyopita yalisambaa baadhi ya maneno yakisema kuwa Wolper amesema kuwa
yeye sio shabiki wa WCB bali shabiki wa Diamond Platinumz tu, hii
ikimaanisha kuwa hana mapenzi na wasanii wengine wa wcb zaidi ya bosi wa
lebel hiyo.
Hata
hivyo Wolper amefunguka na kukanusha kuhusu maneno hayo na kusema kuwa
watu waliomsikia walimuelewa vibaya kwa sababu si hivyo ambavyo
wamefikiria ndivyo alivyomaanisha.
Wolper
anasema kuwa kwa mtu anaelewa mahusianao yake na WCB hawezi kutilia
mashaka swala kama hilo au kufuatilia kwa undani maneno hayo.
"Mtu
akisikiliza kauli kama hiyo na ananijua mimi lazima atashangaa, mimi
sio shabiki wa WCB, how? mimi nilijibu kutokana na swali nililokuwa
nimeulizwa siku ile.kwaio watu wenye akili zao na wanaonielewa hawawezi
kufatilia hivyo vitu."-Alisema Wolper.
Hata
hivyo hivi karibuni Wolper alisema kuwa anaacha kumsapoti msanii
Harmonize ambae alikuwa mpenzi wake hapo zamani kutokana na wivu alio
nao mpenzi mpya wa msanii huyo.


0 comments:
Chapisha Maoni