Ndoa
ya mwanamuziki Alikiba na mchumba wake Amina inatarajiwa kufungwa kesho
alfajiri katika msikiti wa Ummul Kulthum ulioko eneo la Kizingo jijini
Mombasa.
Mama
wa bibi harusi mtarajiwa, Bi Asma Said anasema ndoa hiyo itafungwa
katika msikiti huo uliojengwa na Gavana wa Mombasa, Hassan Joho.
Anasema
baada ya ndoa kufungwa itafuatiwa na sherehe ya kupambwa bibi harusi
ambayo itafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini humo.
Miongoni mwa watu mashuhuri wanaotarajiwa kuhudhuria harusi hiyo ni Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete na Ommy Dimpoz.
Bi
Asma anasema maandalizi yanaendelea vizuri na nyumbani kwa bibi harusi
mwandishi alishuhudia wanawake wakiwa wanajipamba huku wengine
wakijipaka henna.
Alibainisha
kuwa tayari bwana harusi ameingia nchini Kenya huku wadokezi wakisema
kuwa Alikiba alikuwa katika hoteli ya English Point Marina ambapo ni
karibu na nyumba ya bibi harusi iliopo eneo la Kongowea.
“Kijana
ametoka Tanzania na kuja kuoa Kenya mimi sikujua kama mtoto wangu
ataolewa na Alikiba lakini Mungu ndio aliyepanga,” akasema Bi Asma.
0 comments:
Chapisha Maoni