Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA), limeeleza kuwa, baada ya kufanya mahojiano
na msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, wamebaini
kuwa vijana wengi hawana elimu juu ya sheria mpya ya mitandao
iliyowekwa.
Akizungumza
leo Jumatano Aprili 18, Katibu wa BASATA, Godfrey Mngereza amesema kuwa
baadhi ya watu wanaona kama msanii Diamond amelewa umaarufu jambo
ambalo sivyo kama wanavodhani.
“Watu
wanaweza kuchukulia hiyo kwamba Diamond amelewa umaarufu, amelewa
mafanikio. Lakini mimi niseme kama baraza na masimamizi wa wasanii wote,
tusimhukumu mtu kabla hatujamsikiliza wala kuongea nae. Sidhani kama ni
umaarufu uliompelekea Diamond kufanya mambo kama hayo,” ameema
Mngereza.
Mngereza
amesema sababu kubwa ya wasanii na vijana wengi kufanya makosa ya
kimtandao ni kutokana na sheria hiyo kuwa mpya kwao na hivyo kutaka
elimu ya kutosha juu ya sheria hiyo kutolewa ili iweze kueleweka na
kufuatwa.
“Kwa
vijana wengi wa kitanzania ni sheria mpya. Tunahitaji kuwaelimisha
zaidi kwamba kuweka picha au clip za aina hii hazikuongezei umaarufu,”
amesema.
hatua
hii imekuja ikiwa ni siku chache baada ya msanii Diamond kushikiliwa na
Jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano, baada ya kuweka katika mtandao
wa instagram video zinazomuonyesha akiwa katika faragha na mama watoto
wake, Hamisa Mobeto.
Hatua
hiyo iliibua maswali mengi kwa watu mbalimbali wakiwemo mashabiki wa
muziki wake, kwani tukio hilo limetokea siku chahe baada ya kuvuja kwa
video iliyowaonyesha msanii Nandy na Bilnass nao wakiwa katika faragha.
Jambo
hili liliwafanya watu wengi kuibuka na mwaswali, huku wengine wakidhani
ni ‘kiki’ ambayo ingefuatiwa na kuachiliwa kwa wimbo ama video mpya
kutoka kwa wasanii hao.
Hata
hivyo, wasanii hao wote, Diamond, Nandy, Bilnass pamoja na mwanamitindo
Hamisa Mobetto walishikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano
yaliyochukua muda wa saa kadhaa, kisha kuachiliwa kwa dhamana na
kutakiwa kuripoti tena kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni