Waziri
wa Katiba na Sheria, Palamagamba Kabudi ameikosoa kampeni
iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya
kuwasaidia wanawake wenye watoto waliotelekezwa na waume zao na kusema
kwamba ilipaswa kufanyika kwa faragha.
Kabudi
ametoa kauli hiyo leo Aprili 18, wakati Bunge lilipokaa kama kamati
kupitisha bajeti ya wizara hiyo baada ya mbunge wa Ulanga, Goodluck
Mlinga kuhoji uhalali wa kampeni hiyo.
Profesa
Kabudi amesema shughuli hiyo inaweza kuleta hali ya sintofahamu na
akabainisha kuwa inapaswa kufanyika kwa faragha si kama inavyofanyika
sasa.
Wakati
Kabudi akisema hayo, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Musukuma amesema
kampeni ya Makonda ni ishara ya kukosa kazi ya kufanya.
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema kampeni hiyo ni sahihi ila kasoro yake ni kutokuwa na faragha.
0 comments:
Chapisha Maoni