Hitmaker
wa ngoma ‘Kivuruge’, Nandy a.k.a African Princess amesema moja ya vitu
asivyovipenda katika muziki wake ni kuingia katika beef na msanii
mwingine.
Muimbaji huyu ameiambia Clouds TV kuwa yeye sio msanii wa kupenda ugomvi na yeyote anayetaka ugomvi kwake huwa anampuuzia.
“Mimi sio mtu wa ugomvi wa mara kwa mara kwa hiyo sitamani kuingia kwenye ugomvi na mtu.
"
Huwa napuuzia kwa kumuonyesha kuwa anachokifanya ni cha kijinga
sifuatili, yaani Simuonyeshi kuwa nimeshtushwa na kitu ambacho
anakifanya au labda nakifuatilia,” amesema Nandy.
Utakumbuku
kumekuwa na stori zinazodai kuwa Nandy na Ruby wana beef, hata hivyo
wote wawili wamekuwa wakikanusha hilo kila wanapoulizwa na vyombo vya
habari.


0 comments:
Chapisha Maoni