Naibu
Spika, Tulia Ackson amewatetea mawaziri ambao wanashutumiwa kwa kutumia
vyombo vya habari kujibu hoja za ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti wa
Hesabu za Serikali wiki iliyopita.
Tangu
Alhamisi ya wiki iliyopita, mawaziri wanne akiwamo wa Habari, Utamaduni
na Michezo; waziri wa Fedha na Mipango na waziri wa Viwanda na Biashara
walijumuika na kufanya mkutano na wanahabari wakijibu hoja za ripoti ya
CAG.
Kitendo cha mawaziri hao kilikosolewa na wengi akiwamo Mbunge wa Kigoma Mjini, (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe.
Akizungumza
bungeni leo Aprili 16, Dk Ackson amesema mawaziri hao walikuwa wakitoa
maoni yao kwa vyombo vya habari na si kujibu ripoti ya CAG.
“Kama
ambavyo sheria isivyozuia CAG kuzungumza na vyombo vya habari, hivyo
hivyo sheria haiwazuii mawaziri kutoa maoni yao kwa vyombo vya habari
kuhusu ripoti ya CAG,” amesema Dk Ackson.
Hata hivyo amesema ni wajibu wa maofisa masuhuli kujibu ripoti ya CAG na kuwa hayo yanatakiwa kufanywa na mchakato wa Bunge.


0 comments:
Chapisha Maoni