Mbunge
wa Viti Maalumu Chadema, Devotha Minja ameitaka Serikali kutoa majibu
ina mpango gani kuchukua hatua ili kulinda thamani ya shilingi kama nchi
nyingine zinavyolinda fedha zao.
Mbunge
huyo amesema licha ya kuwepo kwa matamko mengi lakini bado maeneo mengi
Watanzania wanalazimishwa kutumia dola badala ya shilingi ya Tanzania.
Akijibu
swali hilo bungeni leo Jumatatu, Aprili 16, Naibu Waziri wa Fedha na
Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema matumizi ya fedha za kigeni sambamba
na shilingi ya Tanzania yanasimamiwa na Sheria ya Matumizi kwa Fedha za
Kigeni ya 1992.
Dk
Kijaji amesema Desemba 2017 waziri wa fedha alitoa tamko kwa umma kuwa
ifikapo Januari Mosi, 2018, matumizi ya fedha za kigeni yazingatie mambo
halisi yaliyopo na ikiwemo bei zote kutangazwa kwa shilingi ya
Tanzania.
Kuhusu
utitiri wa maduka ya kubadilisha fedha, amesema hadi sasa Serikali
imeshafungia jumla ya maduka 92 na itaendelea kufungia kwa watakaokiuka
sheria ili kulinda shilingi ya Tanzania.
"Mkazi
yeyote wa Tanzania asilazimishwe kulipia bidhaa au huduma yoyote hapa
nchini kwa fedha za kigeni na vyombo vya dola viwachukukie hatua za
kisheria wale wote watakaobainika kukiuka maagizo ya Serikali," amesema
Kijaji


0 comments:
Chapisha Maoni