Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage amefunguka na
kudai serikali ya awamu ya tano huwa haikurupuki katika kufanya mambo
yake kama baadhi ya watu wanavyoendelea kufikilia bali wanafanya mipango
yao kwa kufuata dira na sera.
Waziri
Mwijage ametoa kauli hiyo leo (Aprili 06, 2018) kwenye mkutano wa 11
unaoendelea kufanyika mkoani Dodoma wakati akijibu swali la mbunge wa
Momba Mhe. David Silinde ambaye aliishauri serikali ibadilishe kauli
mbio yake ya kujenga viwanda na kuiita serikali ya kuwezesha mazingira
wezeshi kama baadhi ya viongozi wanavyoendelea kunadi.
"Jambo
linalofanywa na serikali ya awamu ya tano sio la kuamka tu na kufanya,
tunafuata dira ya 2025, tunafuata mpango wa pili wa miaka 5 na tunafuata
maelekezo ya Mhe. Rais Magufuli.
"Serikali
jukumu lake ni kuweka mazingira wezeshi na kazi ya sekta binafsi ni
kujenga viwanda. Sasa sisi serikali ya awamu ya tano tunajenga viwanda,
sisi na sekta binafsi tunakwenda pamoja. Huwezi kutenganisha serikali na
sekta binafsi",amesema Mwijage.
Pamoja
na hayo, Waziri Mwijage ameendelea kwa kusema "Mhe. Silinde rafiki
yangu usisahau, umeme wa Momba kama sio serikali na mimi wakati
nilivyokuwa Naibu waziri wa Nishati usingeweza kufika sasa unapaswa
kushukuru kwa kitego unachokipata ili tuje tukupatie kingine".
Kwa
upande mwingine, Naibu Waziri, Wizara ya Viwanda, Biashara na
Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyanya amewaomba wananchi wa Tanzania
wasitishike katika kuanzisha viwanda nchini vinavyowezekana kulingana na
mahitaji ya maeneo yao.
0 comments:
Chapisha Maoni