Mbunge
wa Ulanga, Goodluck Mlinga (CCM), ameiomba Serikali ipige marufuku
matumizi ya nembo ya Taifa yenye picha ya ya mwanamke na mwanamume (Bibi
na Bwana) kwa sababu mwanamke huyo amevaa wigi hivyo kutoakisi maisha
ya Mtanzania.
Mbunge
huyo ameomba mwongozo wa Spika leo Ijumaa Aprili 6, kwa Mwenyekiti wa
Bunge, Andrew Chenge ambapo amedai katika nembo hiyo kuna bwana amevaa
lubega ambaye anaakisi maisha ya Mtanzania.
“Bibi
aliyevaa wigi haakisi maisha halisi ya Mtanzania hivyo naiomba Serikali
isitishe matumizi ya nembo hiyo na izuie isitumike hadi ifanyiwe
marekebisho kwani bibi amevaa wigi ambalo haliakisi maisha ya
Mtanzania,” amesema Mlinga.
Akijibu mwongozo huo Chenge alihoji iwapo tukio hilo limetokea leo hadi Mbunge huyo anauliza.
“Narudi kwenye kanuni je, suala hili limetokea leo na kama halijatokea leo halipo kwenye kanuni,” amesema.
Amesema kwa sasa wanatakiwa kuheshimu sheria inayosimamia nembo
0 comments:
Chapisha Maoni