Mwenyekiti
wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), (UVCCM), Kheri James
amefunguka na kusema yeye hamtambui wala kumjua mwanaharakati wa
mitandaoni Mange Kimambi na kusema angekuwa anamtambua angeweza
kumzungumzia.
Kheri James amesema hayo alipokuwa kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachorushwa na kituo cha EATV.
Mbali
na hilo Kheri James alidai kuwa yeye hatambui wala kufahamu juu ya
maandamano ya nchi nzima ambayo yanahamasishwa kupitia mitandao ya
kijamii ambayo yanadaiwa kufanyika April 26 mwaka huu.
Hata
hivyo Mwenyekiti huyo wa wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi,
Kheri James amewalalamikia baadhi ya watanzania na wapinzani ambao
wamekuwa wakiisema na kuitangaza nchi kwa mambo mabaya yaliyopo ndani
Amesema
jambo hilo ni baya sana kwani litaleta athari kubwa kwani wawekezaji,
watalii watahofia kufika nchini kwetu jambo ambalo litafunga milango ya
maendeleo ya nchi.
0 comments:
Chapisha Maoni