Naibu
Spika wa Bunge Dk. Tulia Akson ameitahadharisha Serikali kuwa makini na
kampuni ya Philips ambayo imeingia nayo mkataba wa kutoa huduma za
XRays nchi nzima kwa madai kwamba ni wasumbufu.
Naibu
Spika ametoa kauli hiyo jana wakati Naibu Waziri wa Afya Dk. Faustine
Ndugulile alipoweka wazi kuwa Serikali inatarajia kuingiza nchini
machine 34 za kisasa za XRay ambazo zitaletwa na kampuni hiyo ya
Philips.
Dk.
Tulia alisema kuwa kampuni hiyo ilisumbua sana katika tenda ya
Hospitali ya Mafia, iliyosababisha Mafia kutokuwa na Mashine mwaka mzima
hivyo kuiomba wizara kujipanga vizuri kwani wana usumbufu mkubwa.
Akitaka
kupata uhakika juu ya kampuni hiyo Dkt. Tulia alisema; "Mh. Naibu
Waziri naomba utufafanulie vizuri kampuni hii ndiyo ile iliyowasumbua
hospitali ya Mafia kwa mwaka mzima ni hawa philips au siyo hawa?
"Kama ni hawa utatufafanulia baadaye lakini kama ni hawa wameshatusumbua sana. Mbunge wa Mafia ameshazungumza sana humu ndani".
Akifafanua
kuhusu kampuni hiyo Naibu Waziri wa Afya alisema kuwa serikali kupitia
wizara imeingia mkataba wa utoaji wa huduma za Xrays nchi nzima na
kampuni hiyo pasipo kukweka wazi kama ndiyo hiyo kampuni
inayolalamikiwa.
0 comments:
Chapisha Maoni