Mbunge
wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo amefunguka na kuonyesha
kuchoshwa na baadhi ya mambo ambayo yanaendelea nchini na kuamua
kuwaomba wazee wa Ujiji Kigoma wakae ili kuweza kumaliza mambo hayo
anayodai ni ya kipuuzi.
Zitto
Kabwe amesema hayo baada ya Idara ya Uhamiaji kumuhoji kuhusu uraia
wake Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania, Abdul Nondo
jambo ambalo Zitto Kabwe anasema idara ya uhamiaji inatumika kisiasa
dhidi ya mwanafunzi huyo.
"Sio
kosa hata kidogo Abdul kuzaliwa Ujiji Kigoma. Imekuwa tabia ya Serikali
kuwapa kesi za uraia watu wanaotoka mikoa ya magharibi hasa Kigoma.
Suala la Nondo ni vita dhidi ya Watu wa Kigoma. Tutapambana.
Tutampigania Abdul Nondo. Watanzania tusikubali upuuzi huu wa watu wa
Uhamiaji kuwafanya raia wa mikoa kama Kigoma kuwa raia wa daraja B"
alisema Zitto Kabwe
Aidha
Zitto Kabwe alikwenda mbali na kusema kuwa mwanafunzi huyo ni mjukuu wa
moja ya muasisi wa TANU ambaye pia alipigania uhuru wa Tanganyika
"Abdul
Nondo Abdul Omar Mitumba, mjukuu wa Marehemu Mzee Omar Mitumba, mwasisi
wa TANU na mpigania Uhuru wa Tanganyika leo anaitwa na maafisa Uhamiaji
eti kuhojiwa uraia. Hao maofisa uhamiaji na aliyewatuma hawana
'credentials' ambazo Babu yake Nondo, Mwenyekiti wa TSNP anazo. Wazee wa
Ujiji sasa mkae. Tumalize haya mambo ya kipuuzi" alisisitiza Zitto
Kabwe
Mwanafunzi
Abdul Nondo aliitwa jana idara ya uhamiaji kuhojiwa juu ya uraia wake
na kujaza fomu hivyo anapaswa kufika tena ofisi za uhamiaji tarehe 20
mwezi huu kwa ajili ya kupeleka vyeti vya kuzaliwa yeye, baba na mama
yake, na bibi na babu kwa pande zote mbili za wazazi wake
0 comments:
Chapisha Maoni