Wiki
ya kwanza ya mwezi Oktoba hujulikana kama wiki ya huduma kwa mteja na
huadhimishwa duniani kote. Benki ya NMB imeamua kuendelea kusherehekea
huduma kwa mteja kwa mwezi mzima ili kuonyesha jinsi inavyomjali mteja
kibiashara, kimaendeleo pamoja na amani kwa ujumla. NMB imejikita kwenye
kutoa huduma bora zinazofikia malengo ya wateja wa ndani na nje.
Kutana
na Meneja Mwandamizi wa huduma kwa wateja wa NMB, Amanda Feruzi
anayetuelezea maoni binafsi na ya kampuni kuhusu huduma kwa mteja na
kwanini ni muhimu kuadhimisha huduma kwa mteja.
Mimi: Karibu sana Amanda, tuanze kwa kufahamu jukumu lako ni nini?
Amanda: Jukumu langu ni kutengeneza, kuratibu, kufuatilia na kupima ubora wa huduma kwenye benki
Mimi: Huduma kwa mteja inamaanisha nini kwako na kwenye benki kwa ujumla?
Amanda: Binafsi,
naamini kwamba huduma kwa mteja ni kuwaheshimu na kuwajali wateja kwa
kutumia weledi kufanikisha mahitaji yao. Kama shirika – huduma kwa
wateja ni jambo la msingi sana hapa NMB na ndio maana kila siku
tunaboresha huduma na bidhaa zetu ili kufanikisha malendo ya wateja
wetu.
Mimi: Kwanini ni muhimu kuwa na wiki ya huduma kwa mteja?
Amanda: Wateja
wetu (wa ndani na nje) ndiyo sababu ya sisi kuwa na mafanikio. Kwahiyo,
tunasherehekea mchango wao na kuwaahidi kwamba TUNAWAJALI kwa kuwa
sehemu ya mafanikio yetu.
Mimi: Ni kitu gani cha muhimu sana cha kufuata unapokuwa unamhudumia mteja?
Amanda:
Kitu cha msingi sana wakati wa kumhudumia mteja ni kuhakikisha mahitaji
na matarajio yake yanafikiwa. Inapotokea kwamba kwa namna moja au
nyingine hatujafikia matarajio ya mteja wetu, tunachukua mrejesho na
kulifanyia kazi suala hilo.
Mimi: Msemo wa “mteja ni mfalme” una ukweli kiasi gani?
Amanda: Tunaposema
mteja ni mfalme, tunarudi palepale kwenye kutilia msisitizo wa
kusherehekea wiki ya huduma kwa mteja. Mteja ni mfalme kwa sababu ndiye
sababu ya sisi kufanikiwa na kuongeza jitihada ili kufanikisha malengo
yake. Mteja anahitaji huduma bora kwenye pesa zake hivyo, ni wajibu wetu
kumsikiliza kwa makini, kumwelewa na kufanikisha mahitaji yake.
Mimi: Kama huduma kwa mteja ingekuwa ni mnyama, unafikiri angekuwa ni mnyama gani na kwanini?
Amanda: Hilo
ni swali zuri lakini gumu pia. Mi nafikiri ningefananisha wiki ya mteja
na tembo. Tembo ni wapole na viongozi wasiotumia mabavu. Hiyo ndio
sababu tembo wenzao huwaheshimu kutokana na uwezo wao wa kutatua
matatizo. Hiyo ni sawa na hhuduma kwa mteja.
Mimi:
Ahsante sana kwa kuzungumza nasi kuhusu huduma kwa mteja na namna
mlivyojipanga kuhakikisha kwamba mnatimiza matarajio ya wateja wenu.
Amanda: Shukrani sana.