Leo
April 19, 2018 Meneja wa Fedha wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA),
Prosper Kimaro amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
akikabiliwa na kosa la kujilimbikizia mali zenye thamani ya Shilingi
Bilioni 1.4 zisizolingana na kipato chake halali.
Kimaro
anadaiwa kumiliki nyumba zenye thamani ya Bilioni 1,178,370,334,
zilizopo maeneo ya Temeke DSM na magari 7 yenye thamani Shilingi Milioni
307,364,678.20.
Kimaro
amesomewa mashtaka yake na wakili wa serikali, Vitalis Peter mbele ya
Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo amedai kuwa mshtakiwa anakabiliwa
na kosa moja.
Wakili
Vitalis amedai mshtakiwa anakabiliwa na kosa la kujilimbikizia mali
zisizolingana na kipato chake ambapo anadaiwa amelitenda kosa hilo kwa
miaka tofauti kati ya 2012 na 2016.
Anadaiwa
mali hizo amejilimbikizia maeneo ya Temeke DSM akiwa mtumishi wa umma
wa TPA kama Meneja wa Fedha, amekutwa na mali zisizolingana na kipato
chake halali cha zamani na cha sasa.
Mali
hizo ni nyumba 2 zilizopo mtaa wa Uwazi Temeke (Mil 124.2), kiwanja
kimoja kilichopo Yombo Vituka (Mil.12.9), nyumba 2 zilizopo Temeke (Mil
63.5).
Pia
nyumba nyingine 3 zilizopo Temeke zenye thamani ya (Mil.159), nyumba
nyingine 3 zilizopo maeneo hayo (Mil 170.1), nyumba nyingine moja (Mil
71.3).
Pia
ana kiwanja Temeke (Mil 35), kiwanja kingine (Mil 25) na kujenga nyumba
3 (Mil 159), pia nyumba nyingine moja (Mil 106), pia nyumba nyingine 3
zilizopo Temeke zikiwa na thamani ya (Mil 214).
Pia ana nyumba 4 zilizopo Viziwa Ziwa Kibaha Mjini (Mil 199.7), nyumba nyingine Kilimahewa Tandika (Mil 70).
Pia
anamiliki magari aina ya Toyota Land cruise (Mil 180.1), Mitsubishi
(Mil 38.4), Massey Ferguson (Mil.24), Trailer (Mil 4.5), Toyota Harrier
(Mil 35.8), Trailer (Mil 4.8), Massey Ferguson (Mil 19.1).
Baada
ya kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa alikana makosa yake ambapo Wakili
Vitalis amedai upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika, pia hana pingamizi
na dhamana.
Hakimu
Simba ametoa masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini 2
watakaowasilisha hati ya mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh.Mil
200, pia mshtakiwa asitoke nje ya mkoa wa Dar es Salaam bila kibali
pamoja na kuwasilisha hati zake za kusafiria.
Mshtakiwa huyo hajatimiza masharti ya dhamana, ambapo Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi May 3,2018.
0 comments:
Chapisha Maoni