Mbunge
wa Mchinga (CUF), Hamidu Bobali amesema ndege za Shirika la Ndege
Tanzania (ATCL), kutoa huduma za usafiri wa anga asubuhi hadi jioni na
kusitishwa usiku hakiwezi kulinufaisha shirika hilo, huku akifananisha
kitendo hicho na huduma za usafiri wa daladala.
Akizungumza
bungeni Aprili 24, 2018 katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano mwaka 2018/19, Bobali alisema hakuna anayepinga
shirika hilo kufufuliwa lakini tatizo ni uamuzi wa Serikali kununua
ndege bila kuboresha miundombinu na kuwa na mipango endelevu.
“Tunapaswa
tuelewane hakuna anayekataa wala kupinga ATCL kufufuliwa. Tunachopenda
kushauri ni namna na njia inayotumika kulifufua shirika. Mawaziri mpo
hapa mnasoma ripoti mbalimbali za mashirika ya anga ya kimataifa na
mnajua nini kinaendelea kwenye mashirika ya ndege mengine,” alisema.
“Kwa
sasa takwimu zilizopo, kwa mwaka mmoja mashirika ya ndege duniani
yanapata hasara ya Dola 8 bilioni za Marekani, kwa Afrika pekee mwaka
uliopita mashirika ya ndege yalipata hasara ya Dola 600 milioni za
Marekani. Ikiwa hali ndio hii tukienda kuifufua ATCL lazima tuwe na
tahadhali.”
Alisema
katika mjadala huo, baadhi ya wabunge wamehoji kitendo cha ndege za
ATCL kutoa huduma, huku viwanja vya ndege nchini vikiwa vibovu na hakuna
usafiri wa usiku wa ndege.
“Wakati
tunanunua ndege tulijua tunasafiri nje ya nchi, lakini najua kusudio la
kununua ndege ni zitumike ndani, kwanini zaidi ya viwanja vya ndege
asilimia 70 nchini havina taa?” alihoji.
0 comments:
Chapisha Maoni