Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa jana
amepangua hoja wa wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya bajeti ya
wizara hiyo huku akithibitsha kuwa Serikali inatarajia kununua ndege
nyingine kubwa ya saba ya masafa marefu.
Alisema Serikali haikurupuki kununua ndege hizo kwa kuwa inao mpango kazi unaobadilishwa kila mara kulingana na wakati.
“Serikali itaendelea kununua ndege na haitakodi kwa sababu kukodi ni gharama kubwa ikilinganishwa na kununua.
“Nia
ya serikali ni nzuri kwani huwezi kuwa na viwanja vya ndege kama huna
shirika lako la ndege, hivyo tumenunua ndege sita ambazo tatu zimetua na
zinafanya kazi.
"Mwaka
huu tunategemea ndege tatu zitawasilisha ambazo ni Boeng 787 ya masafa
marefu yenye uwezo wa kuchukua abiria 262, nyingine mbili zenye uwezo wa
kuchukua abiria 132 kila moja ni Bombardier CHCS 300 ambazo zitawasilia
na kuanza kufanya kazi.
“Kikawaida
huwezi kuwa na ndege moja ya masafa marefu ikafanya kazi vizuri hivyo
kwenye bajeti hii tumeshapanga kununua ndege nyingine boeng 787 ili tuwe
na ndege mbili za masafa marefu ambapo moja ikiwa inatoka Dar es Salaam
kwenda Guangzhou na moja inatoka Guangzhou kuja Dar es Salaam. Ndio
utaratibu unavyokwenda,” amesema.
Aidha,
amesema kwamba Kampuni ya Ndege (ATCL), inao mpango kazi hivyo si kweli
kwamba haina kama wabunge walivyodai ambapo kila baada ya muda
inabadilishwa kwani si msahafu hivyo itabadilishwa kutokana na mahitaji
ya soko.
0 comments:
Chapisha Maoni