Katika
hatua isiyo ya kawaida leo Bungeni Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini
ametoa mwongozo akitaka viti vya bungeni kukarabatiwa kwa kuwa viti
hivyo ni vibovu na vinawapa shida wabunge.
Salasini
ameyasema hayo kwenye kipindi cha Maswali na majibu huku mwongozo wake
ukiitaka serikali itoe majibu ni lini viti hivyo vitakarabatiwa ili
kuwaondolea adha wabunge wakati wa vikao.
''Mh.
Spika viti hivi tunavyokalia havipo kwenye hali nzuri kabisa,
vimechakaa na havifanyiwi marekebisho na leo kiti changu kimenifinya
makalio. Je ni lini vitafanyiwa ukarabati ?,'' amesema Selasini.
Baada ya kuomba muongozo huo Spika wa Bunge Mh. Job Ngudai amesema kuwa suala hilo limepokelewa na litatolewa ufafanuzi.
0 comments:
Chapisha Maoni