Mbunge
wa Viti Maalumu, Kiteto Koshuma ameitaka serikali kutamka wazi kuwa
wanawake walioolewa chini ya miaka 18, ndoa zao ni batili.
Koshuma ametoa kauli hiyo leo Aprili 18 bungeni wakati akichangia hotuba ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka 2018/19.
Amesema sheria ya ndoa ya Tanzania ya mwaka 1972 inakwenda kinyume makubaliano ya kimataifa.
Mbunge
huyo ametoa masikitiko kuwa serikali haiwatendei haki wanaharakati
ambao walipeleka kesi ya kupinga sheria hiyo mahakamani na wakashinda
lakini serikali imekata rufaa.
0 comments:
Chapisha Maoni