Mtu
mmoja amefariki dunia na wawili kujeruhiwa baada ya kukatana kwa visu
na mapanga katika ugomvi unaohusishwa na wivu wa mapenzi uliotokea
katika Kitongoji cha Kirenero wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mara, Juma Ndaki alisema tukio hilo limetokea jana
Aprili 17, 2018 asubuhi katika kitongoji cha Kirenero kijiji cha
Kichongo wilayani Serengeti mkoani Mara.
Amemtaja
aliyefariki kuwa ni Kibure Samwel (39) ambaye alichomwa kisu tumboni na
kifuani wakati Nyang’anyi Waitara (44) mkazi wa Itununu, katika tukio
hilo alikatwa mkono.
Munge Samwel (44) kaka wa marehemu alikatwa pajani na mtuhumiwa.
Amesema chanzo ni wivu wa mapenzi kwa kuwa mwanamke ambaye awali alikuwa mke wa Waitara kwa sasa ameolewa na Munge.
Kamanda
huyo amesema tangu mwanamke huyo ambaye hakutajwa jina aolewe na Munge
kumekuwa na mgogoro baina yao kuhusiana na hilo, na walipokutana
inadaiwa walianza kushambuliana kwa maneno kisha kuanza kukatana.
“Aliyekufa
ni mdogo wake na Munge Samwel ambaye katika ugomvi huo alifika kwenye
tukio na kukuta kaka yake anashambuliana kwa silaha na Waitara, akaamua
kuchukua panga kumsaidia ndipo mtuhumiwa akamchoma tumboni kisha kifuani
na kufa papo hapo,”alisema.
Mwenyekiti
wa Kitongoji hicho, Joseph Mwita alisema mgogoro huo ni wa muda mrefu
ambapo Waitara alimshutumu Munge kuwa chanzo cha mgogoro wa ndoa yake
mpaka mke akamfikisha mahakamani na kuomba talaka.
“Waitara
(mtuhumiwa) aligoma kurudishiwa mahari na Munge ili amchukue mke wake
kwa madai kuwa ameshazaa naye watoto watatu, hali iliyomlazimu Munge
kumhamishia mwanamke huyo Tarime kwenye mji wake mwingine,” alibainisha.
0 comments:
Chapisha Maoni