MWIGIZAJI bora wa kike katika tasnia ya filamu nchini Tanzania Wema Sepetu amesaini mkataba mnono na Kampuni ya Auguster kwa ajili ya usambazaji wa filamu yake ya Heaven Sent.
Mkataba huo umesainiwa leo katika mkutano uliofanyika ndani
ya studio za Azam TV jijini Dar es Salaam, ambapo kampuni hiyo
imewakilishwa na Ofisa Uhusiano wake Nembris Soka.
Tukio pia limeshuhudiwa na mwandishi na muongozaji wa filamu hiyo, Neema Ndepanya.
Kwa upande wa Wema amesema tangu kutolewa rasmi kwa filamu
hiyo, wapenzi wake wamekuwa wakiipata kupitia ‘Application’ ya Wema
Sepetu, na hapakuwa na DVD zozote ambazo zilikuwa zikisambazwa kwa watu.
Amesema kampuni hiyo imeamua kufanya kazi hiyo baada ya
filamu hiyo kushinda tuzo mbili katika Tuzo za Kimataifa za Filamu
(SZIFF) zilizofanyika Aprili MOSI, mwaka huu katika Ukumbi wa Mlimani
City.
Soka yeye amesema Kampuni ya Auguster wamevutiwa na kiwango
cha filamu hiyo na wameona jinsi mashabiki wa filamu nchini walivyo na
kiu ya kuitazama filamu hiyo, na ndiyo maana wameamua kuifanya kazi hiyo
ya usambazaji ili iwafikie watu.
0 comments:
Chapisha Maoni