Chama
cha ACT-Wazalendo, kimemuandikia barua Spika wa Bunge, Job Ndugai
kikimuomba kufanya uchunguzi maalumu kuhusu kiasi cha Sh1.5 trilioni
ambazo hazionekani kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG).
Katibu
wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu
amesema hayo leo Alhamisi Aprili 19, 2018 wakati akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu ufafanuzi wa kauli na hoja zilizosemwa na
CCM jana.
"Sasa
hivi CCM wakithubutu kutochokoza ACT-Wazalendo, swali letu ni moja tu
Sh 1.5 trilioni ziko wapi? Upinzani tuna wajibu wa kuhoji ili
kuhakikisha Watanzania wanajua fedha zao zinakwenda wapi," amesema.
Shaibu
amesema barua hiyo imeandikwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Jeremiah
Maganja akimuomba Ndugai kutoa kibali maalumu kwa Kamati ya Bunge ya
Hesabu za Serikali (PAC), ikutane na imuagize CAG kufanya ukaguzi kuhusu
fedha ili zijulikane zilizokopelekwa.
"Matumaini
yetu Spika Ndugai atazingatia maombi haya. Lengo letu Watanzania wajue
ukweli kwa sababu kumekuwa na upotoshaji mkubwa ukiendelea kuhusu
fedha hizi," amesema Shaibu.
Amesema
chama hicho hakitarudi nyuma katika sakata hilo na kuwaomba Watanzania
kuwaunga mkono hadi hatua ya mwisho ili kujua ziko wapi kwa sababu ni
fedha nyingi.


0 comments:
Chapisha Maoni