Muigizaji mkongwe wa Bongo movie Dr. Cheni amefunguka mazito juu ya maisha ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ gerezani.
Ni
miezi kadhaa tangu Lulu aende jela baada ya kuhukumiwa miaka miwili
baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia aliyekuwa mpenzi
wake marehemu Steven Kanumba.
Wiki
iliyopita tuliona jinsi Dr. Cheni alivyomuwakilisha Lulu kwa kutoa
msaada kwenye kampenzi ya Namthamini ya EATV. Dr. Cheni ni mtu ambaye
siku zote amekuwa na ukaribu sana na Lulu hadi Lulu humuita Baba yake.
Kwa
mara nyingine Tena Dr. Cheni amefunguka kuhusu maisha ya Lulu gerezani
ambapo kwenye mahojiano na Millard Ayo Tv amefunguka haya:
"Kusema ukweli Lulu ni binti jasiri sana yaani sisi tuliokuwa nje tuna majonzi kuliko yeye mwenyewe
"Yaani
ukienda unamkuta ana furaha mtacheka naye mtafurahi, kikubwa anasema tu
niombeeni basi na kitu kikubwa Lulu huko jela anatizama sana mabinti,
anasema anawapenda sana mabinti wa Kitanzania”.
Lakini
pia Dr. Cheni amesema kuwa Lulu ana kawaida sana ya kutoa misaada
ingawa hapendi kujitangaza Kwenye mitandao ya kijamii pia amedai Miezi
michache kabla hajahukumiwa alienda kutoa msaada segerea.


0 comments:
Chapisha Maoni